4/14/2019

Kutolewa kwa Yondani kwamvuruga Kocha wa Yanga SCBaada ya beki wa Yanga SC,  Kelvin Yondani kutolewa Uwanjani kwa kadi nyekundu Alhamisi iliyopita, kitendo hicho kimemvuruga kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera ambapo sasa analazimika kumuandaa mbadala wake.

Yondani alitolewa Uwanjani kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa ambapo alimpiga mchezaji wa Kagera Sugar.

“Najua nitamkosa Yondani kama mechi tatu hivi na bado timu ina michezo migumu, hivyo katika mapumziko tuliyonayo nitamtengeneza mchezaji atakayecheza nafasi yake ili tuishinde michezo iliyobaki kwenye FA na ligi kuu.

“Lakini pia wakati mwingine waamuzi wanatakiwa kuwa makini, mimi nilikuwa karibu na tukio hilo, nimeona waziwazi kwamba yule mchezaji wa Kagera ndiye alianza kumpiga Yondani na kisha Yondani naye akajibu, nafikiri ndipo mwamuzi akaona lakini kama ni adhabu wote walistahili kupewa.” alisema Zahera
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger