Lulu Atangaza Ujio Wake Kwenye Filamu


Image result for Elizabeth Michael
Msanii wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu' amesema yupo mbioni kurejea rasmi kwenye ulingo wa filamu.

Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds FM amesema kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha ujio wake huo.

"Kwenye movie nitarudi hivi karibuni, nahitaji kukua sehemu zote, sio tu kwenye maisha yangu bali hata kwenye kazi zangu na vitu vingine. Nipo kwenye process ya kurudi kwenye movies na itachukua muda kurudi kwa sababu nataka utofauti na vile nilivyokuwa navifanya zamani kwenye movies," amesema.

Ameendelea kwa kusema, 'Kiukweli kwenye tasnia ya filamu tumeyumba kwa kiasi fulani na hata ukiangalia uzalishaji wa filamu umepungua sasa kama uzalishaji umepungua hata ushirikishwaji wa tuzo za filamu kwa nchi zingine umepungua, Tupo kwenye wakati wa kuboresha tasnia yetu hivyo nina imani mambo yatakuwa sawa mbeleni'.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Lulu Atangaza Ujio Wake Kwenye Filamu Lulu Atangaza Ujio Wake Kwenye Filamu Reviewed by Udaku Special on April 17, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.