4/21/2019

Mtuhumiwa wa Mauaji Atoroka na Kupatikana, Wawili Wanasakwa

Na John Walter-Manyara 

Mtu mmoja mkazi wa Hanang mkoani Manyara  anayetuhumiwa kwa mauaji ya mke na mtoto wake Desemba 2018, iliosababishwa na wivu wa mapenzi ametoroka mikononi mwa  polisi alipokuwa anafikishwa mahakama ya wilaya ya Babati . 


Shamndudi John au kwa jina maarufu Sikukuu Tulway alikamatwa siku iliyofuata katika  wilaya ya Hanang na anaendelea kushikiliwa na polisi na muda wowote atafikishwa Kortini kujibu mashtaka yanayomkabili. 


Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga amesema  April 15 baada ya kesi ya mtuhumiwa  kutajwa akiwa anajiandaa kupanda gari kwa ajili ya kurudishwa mahabusu, ghafla  kwa ku kuwa mahakama hiyo ipo karibu na ziwa Babati ambalo lina majani mengi alikimbilia kuelekea ziwani na juhudi za kumkamata wakati ule zilishindikana akawa ametokomea kabisa. 


Amesema kwamba baada ya hapo operesheni kali ilifanyika na kufanikiwa kuzaa matunda ambapo Aprili 16 waliweza kumkamata mjini Katesh wilaya ya Hanang majira ya  usiku wa manane kwa kushirikiana na wananchi. 


Polisi walipata ugumu wa kumkamata mtu huyo kwani alikimbilia eneo la ziwa Babati huku wakihofia kuwa kumpiga  risasi kungepelekea kuumia watu wasio na hatia.


Katika tukio lingine kama hilo jeshi la polisi linaendelea kuwatafuta Wafungwa wawili waliofanikiwa kutoroka wenye Namba 108/2019 Lekitambi Kambuu [28] na mwenzake mwenye Namba  109/2019 Abirikaa Sokoine [25] wote wakitoka katika Gereza La Babati ambao  walitoroka wakiwa chini ya Ulinzi mkali wa polisi wakati walipokuwa wakisimamiwa na kufanya kazi katika shughuli za ujenzi wa nyumba za askari polisi unaoendelea  huko Mtaa wa  Bagara Babati.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger