Uongo Wamponza,Aafungwa Jela Miaka 20, Polisi Wachoshwa Tatabia Zake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Uongo wamponza, afungwa jela miaka 20, polisi wachoshwa natabia zake
Mwanamume mmoja wa California- nchini Marekani amefungwa miaka 20 jela kwa kuwapigia simu za uongo polisi, ikiwemo simu moja mbayo ilisababisha kuuawa kwa mwanaume asiye na hatia.

Tyler Barriss
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Tyler Barriss alifanya kile kinachoitwa “swatting” ambapo simu bandia hupigwa kwa polisi kwa ajili ya kuwaagiza polisi kutumia silaha na mbinu maalumu, hutumiwa na polisi kuivamia nyumba au makazi yanayolengwa, akidai kuwa alikuwa ameiteka familia yake.

Polisi walipofika eneo la tukio alipowaelekeza, walimpiga risasi baba wa watoto wawili Andrew Finch.


Barriss alikiri kupiga simu baada ya kuhusika katika mzozo juu ya mchezo wa video wa kuwaita polisi na wanaume wengine wawili.

Casey Viner mwenye umri wa miaka 18-kutoka Ohio na Shane Gaskill mwenye umri wa miaka 20-kutoka Wichita kwa pamoja wanasubiri kesi yao juu ya uhusika wao katika tukio hilo.

Tarehe 28 mwezi Disemba Barriss aliwaambia polisi kuwa alikuwa amempiga risasi baba yake na kuiteka familia yake.

Aliipatia polisi anuani ya Kansas ili hali anuani hiyo ilikuwa Los Angeles, umbali wa maili 1,400.

Tyler Barriss
Polisi waliojihami kwa silaha walikwenda kwenye makazi hayo na kumpiga risasi Andrew Finch mwenye umri wa miaka 28- ambaye hakuwa na hatia wala kuhusika katika mzozo wa mchezo wa video wa kuwaita polisi.

Polisi imesema kuwa afisa wake alimpiga risasi Bwana Finch, baada ya kusogeza mikono kwenye nyonga yake.

Maafisa wa polisi wa kikosi cha dharura ambalo hufahamika kama -Swat miongoni mwa maafisa wa usalama
“Ninatumai kwamba mashtaka haya na ukubwa wa hukumu vinatuma ujumbe ambao utamaliza mchezo wa ‘kuwapigia polisi simu za dharura za uongo ‘ katika jamii zenye mchezo huo, na pia dhana nyingine za aina hiyo ,” Alisema mwanasheria wa Kansas- Stephen McAllister katika kauli yake.

Barriss pia alikiri kupiga simu nyingine za uongo, ikiwemo simu kuhusu tisho la ugaidi kwenye makao makuu ya shirika la ujasusi la Marekani FBI.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad