Urusi: Marekani ina uwezo wa kutizimia INTERNET Wakati Wowote Ikitaka Ndio Maana na sisi Tunajiandaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bunge la Urusi limepitisha muswada ambao ukiwa sheria basi Taifa hilo lenye Watu zaidi ya M.140 litaunda INTERNET yake peke yake na kuachana na inayotumika duniani

Muswada huo uliopitishwa kwa kura nyingi za wabunge 307 huku 68 wakiupinga, utawasilishwa katika Bunge Kuu la Urusi ili kuidhinishwa na kisha kuwasilishwa kwa Rais Vladmir Putin kutia sahihi ili kuufanya sheria kamili na kuanza kutekelezwa Novemba, mosi.

Sheria hiyo itawezesha Serikali ya Urusi kubuni miundombinu yake binafsi ya Intaneti na kuweza kusalia mtandaoni hata kukitokea dharura ya taifa lolote kujaribu kuuzima.

Mmoja wa waandishi wa muswada huo, Andrei Klishas aliliambia Shirika la Habari la Ujerumani (DW) kuwa hawana shaka Marekani ina uwezo wa kiufundi wa kuizimia Urusi huduma za intaneti wakati wowote wakipenda, hivyo wanajiandaa kiufundi kuhakikisha wanajilinda dhidi ya mashambulizi kama hayo.

Hadi sasa maswala ya kiufundi ya namna miundombinu hiyo itakuwa hayajakuwa bayana, lakini taasisi kuu ya mawasiliano ya Urusi – Roskomnadzor ndiyo itakuwa kituo kikuu cha kufuatilia na itasimamia intaneti hiyo kukitokea mashambulizi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad