5/21/2019

Rais Magufuli I Love you, ilikuwa Ndoto Kukutana na Wewe - Sheikh KipozeoShekh Hilal Shaweji (Shekh Kipozeo) amemuambia Rais John Pombe Magufuli anampenda sana kutokana na juhudi anazozifanya.

Amesema wakati Magufuli akiingia madarakani kulikuwa hakuna ndege hata moja lakini hadi hivi sasa zimefika nane hivyo ana kila sababu ya kumuambia nampenda.

“I love you so much, ilikuwa ni ndoto yangu kukutana na wewe ili nikuambie maneno haya leo niko mbele yako naomba nikuambie hivyo.”

“Nilipata nafasi ya kuzionja ndege hizo, nilipanda kwenda Mwanza na kurudi na nikapanda kwenda Burundi, Mwenyezi Mungu akubariki  sana mzee wetu pamoja na viongozi wetu,” amesema Kipozeo.

Shekh Kipozeo ameyasema hayo leo katika hafla ya Shirika la SimuTanzania (TTCL) kutoa gawio kwa Serikali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger