"Sekta Yetu ni Ngumu" - Waziri Mkuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

"Sekta Yetu ni Ngumu" - Waziri Mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waongeze kasi ili utendaji kazi serikalini uweze kufikia hatua nzuri.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo alipokutana na viongozi na watumishi wa ofisi yake na kufuturu nao pamoja kwenye makazi yake jijini Dodoma.

“Ninawashukuru watumishi wote kwa ushirikiano mnaotupatia mimi pamoja na mawaziri wenzangu, makatibu wakuu wote watatu, Wakurugenzi mbalimbali na wakuu wa vitengo. Tunatakiwa tuongeze kasi ili tufikie hatua nzuri ya utendaji kazi serikalini”,amesema Waziri Mkuu

Aidha amesema utendaji kazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mgumu kwa sababu unahusika na usimamizi wa shughuli za Serikali nzima na watendaji wote wa Serikali.

"Sekta yetu ni ngumu kwa sababu sisi ni wasimamizi wa Serikali na watendaji wote wa Serikali. Tuna wajibu wa kuwaunganisha watendaji wa wizara zote serikalini”, ameongeza Waziri Mkuu.

“Sisi sote ni watumishi wa umma, kwa hiyo mchango wenu una maana kubwa na unachangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Serikali nzima. Ninawapongeza kwa utumishi mwema na wenye uadilifu”.amesema Waziri Mkuu
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad