Amunike afanya mabadiliko kikosi cha Taifa Stars

Taarifa kutoka Misri zinaeleza kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amefanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi chake siku chache kabla ya michuano ya AFCON 2019 kuanza nchini Misri.


Amunike amelamika kumrejesha kikosini mlinzi wa kati wa klabu ya soka ya Azam FC kuziba na nafasi ya beki mwingine wa Azam FC Aggrey Morris.

Aggrey Morris alipata majeraha katika mchezo wa kirafiki wa Taifa Stars dhidi ya Misri uliopigwa Alhamis Juni 13, 2019 kwenye uwanja wa Borg El Arab jijini Cairo.

Mchezo huo ulimalizika kwa Tanzania kukubali kichapo cha goli 1-0 ambalo lilifungwa Ahmed Elmohamady dakika ya 64.

Morris aliumia dakika ya 74 na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Mtoni.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments