AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Azizi ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alikutwa ameshafariki dunia akiwa amening'inia katika mti wa mlimau uliopo nyumbani kwake eneo la Kijichi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Zanzibar, Muhammed Hassan Haji, alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana.
“Alikutwa amefariki dunia akiwa ananing'inia katika kitanzi kilichofungwa katika mti wa mlimau uliopo nyumbani kwake Kijichi,” alisema.
Alisema kifo chake ni pigo na pengo kubwa kwa Jeshi la Polisi.
Aliitaka familia ya marehemu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Juma alizaliwa mwaka 1960 huko Michakaeni kijijini kwao kisiwani Pemba. Alizikwa jana jioni katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK