Mbowe, Zitto watua Mahakama ya Afrika Mashariki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Viongozi wote wakuu wa upinzani nchini Tanzania akiwepo, Freeman Mbowe, Maalim Self Sharif Hamad na Zitto Kabwe wametua katika Mahakama ya Afrika Mashariki ambapo wamehudhuria kesi ya kupinga  sheria mpya ya vyama vya siasa.

Katika kesi hiyo ambayo viongozi wa upinzani wanawakilishwa na Mawakili Fatuma Karume, John Mallya na Jebra Kambole wanaomba mahakama kusitisha sheria hiyo.

Wakili Karume  ameeleza majaji wa mahakama hiyo leo Jumatano Juni 19, 2019 kuwa sheria hiyo inakiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika masuala ya haki na demokrasia.

Amesema miongoni mwa upungufu katika shauri hilo ni kuzuia viongozi wa upinzani kutoa elimu ya mpiga kura bila idhini ya msajili wa vyama vya siasa, kuzuia walinzi binafsi ya vyama na kuingiliwa uhuru wa vyama.

Majaji wa mahakama hiyo bado wanasikiliza maombi ya upinzani kutaka mahakama hiyo kutoa uamuzi wa dharura kuzuia baadhi ya vifungu vya sheria hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad