Njombe Wafanya sherehe Katika Kusimamia Zoezi la Ukusanyaji Mifuko ya Plastiki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe  imeendelea kutekeleza  kwa vitendo agizo la serikali la kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mifuko ya plastiki  katika kata zake zote ikiwa ni kuunga mkono katazo la matumizi ya mifuko hiyo ili kuhifadhi mazingira.


Mapokezi ya wananchi juu ya katazo hilo yamekuwa makubwa, ambapo watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na watu wengine wamejitokeza kwnenye kampeni maalumu ya wilaya, wakiimba nyimbo mbalimbali huku wakisalimisha mifuko yao.

Zoezi hilo limesimamiwa na viongozi wa halmashauri akiwemo Afisa Mazingira wa Wilaya ili kuhakikisha mifuko ya plastiki, maarufu kama 'rambo' ikikusanywa pamoja na wananchi kupewa tahadhari juu ya adhabu kali kwa yeyote atakayebainika kuwa na mifuko hiyo.

Ally Kassinge ni Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe ambae anasimamia zoezi la ukusanyaji wa mifuko ya rambo katika kata zote za wilaya hiyo huku akitoa angalizo kwa raia atakae bainika na mifuko ya rambo katika maeneo yoyote ndani ya wilaya yake.

Zoezi hili la usalimishaji wa mifuko ya Rambo lina ambatana na zoezi la zoezi la kufanya usafi wa mazingira na leo katika maeneo mbali mbali wilayani humo, ambapo usafi huo umechukua nafasi  katika maeneo yanayoizunguka hospitali hiyo teule ya Ilembula.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad