+18..Ukimfanyia Haya Mpenzi Wako,Hata Iwe Vipi Hatokusahau Kamwe...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.

2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.

3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali

4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.

5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.

6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini

7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.

8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.

9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.

10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa pia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad