Bondia Afariki Baada ya Kupigwa Vibaya Ulingoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bondia raia wa Urusi Maxim Dadashev ameaga dunia baada ya pambano lake na Subriel Matias kumsababishia majeraha makubwa ya ubongo.

Dadashev mwenye miaka 28, alishindwa kutembea mwenyewe baada ya pambano hilo ambalo mkufunzi wake Buddy McGirt alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali bila majibu.


Madaktari waligundua kuwa damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo na kufanyiwa upasuaji wa haraka, lakini akafikwa na umauti jana Jumanne.

Pacquiao ashinda ubingwa wa dunia akiwa na umri wa miaka 40
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 24.07.2019
Zidane: Gareth Bale 'anakaribia' kuondoka
Shirikisho la ndondi la Urusi limesema tayari uchunguzi umeshafuguliwa juu ya mkasa huo.

Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Umar Kremlev amedai kuwa kulikuwa na "aina fulani ya uvunjwaji wa taratibu", na kuongeza kuwa: "Tumempoteza Maxim Dadashev. Ilikuwa ni nyota yetu inayochipua.

"Tutaiunga mkono familia yake, ikiwemo kifedha. Tutakamilisha uchunguzi wa kuangalia mzaingira ya pambano, tunahitaji kujua ukweli wa kilichotokea.

"Hili linaweza kutokea kwenye mchezo wowote. Naamini kuna mapungufu ya kibinadamu yamechangia, kulikuwa na aina fulani ya uvunjwaji wa taratibu."

Dadashev ambaye alikuwa akifanya shughuli zake za masumbwi nchini Marekani alishinda mapambano yake yote 13 aliyoyacheza kabla.

Ijumaa alipambana na Matias kutoka Puerto Rico katika jimbo la Maryland ambapo alisukumiwa makonde mazito na kwa kasi kali.

Mkufunzi wa Dadashev, Bw McGirt alieleza baada ya pambano kuwa "alishindwa kumshawishi" kukubali kushindwa, lakini akaamua kurusha taulo ulingoni baada ya kuona "akipigwa zaidi za zaidi kwa makonde ya wazi kadri pambano lilivyokuwa likiendelea."
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad