IGP Afunguka Kuhusu Sauti za 'Nape, Kinana'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema wanafanya uchunguzi wa sauti zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii, zinazodaiwa ni za baadhi ya viongozi wa wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali.


Akizungumza na EATV/EARadio Digital, IGP Simon Sirro amesema wameziona sauti hizo na wameanza kuzifanyia uchunguzi japo hajafahamu uchunguzi huo utakamilika baada ya muda gani na endapo itathibitika kuna makosa ya jinai, watuhumiwa watachukuliwa hatua za kisheria.

"Ni kweli hata sisi hizo sauti nimezisikia na tunafuatilia ili kujua ukweli wake, tukibaini kama kuna kesi ya jinai na kama yaliyokuwa yakitamkwa ni kweli basi tutachukua hatia za kisheria", amesema.

"Kuhusu uchunguzi utakuwa muda gani mimi sijui, inategemea shauri lenyewe", ameongeza IGP Sirro

Wakati huohuo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kupitia msemaji wake, Semu Mwakyanjala, akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, ameeleza kuwa suala hilo wamewaachia Jeshi la Polisi.

"Uhalifu wowote unaoripotiwa na TCRA watu wanaoshughulika na hilo ni Jeshi la Polisi, ila ninachosema kama kuna kosa la jinai, muhusika ashirikiane na Jeshi la Polisi ili ukweli ufahamike", amesema Mwakyanjala.

Hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kulisambaa baadhi ya sauti zilizodaiwa kuwahusisha baadhi ya viongozi mbalimbali waliowahi kuwa ndani ya Serikali akiwemo Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Abdulrahmani Kinana, Waziri mstaafu wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Yusuph Makamba  na Nape Nnauye, zikizungumzia mambo mbalimbali ya serikali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad