Serikali Imesema Bado Haijajua Kama Azory Amekufa au Yupo Hai Wanaendelea na Uchunguzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbas amesema mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Mwandishi wa habari wa Mwananchi, Azory Gwanda amekufa ama yupo hai na kwamba vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi.

Abbas aliyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa :”Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuliwa kimakosa mahojiano yangu kwenye Kipindi cha BBC FOCAS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba Azory Gwanda amefariki dunia,”

Awali Waziri Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi alidai kuwa mwandishi wa habari wa Mwananchi, Azory Gwanda, alitoweka na kufariki.

Kauli hiyo ilizua utata katika mitandao ya kijamii huku wengine wakihoji waziri huyo amejuaje kama mwandishi huyo amefariki.

Waziri Kabudi aliyasema hayo wakati wa mahojiano na BBC katika kipindi cha FOCUS ON AFRICA mjini London waziri Kabudi alinukuliwa akisema kwamba visa vya watu kutoweka vimesababisha uchungu mwingi nchini humo.

“Wacha nikwambie unapozungumzia kuhusu kisa hicho, ni mojawapo ya visa ambavyo vimesababisha uchungu mwingi nchini Tanzania”.

Aliongezea kuwa :”Katika eneo la Rufiji sio tu Azory Gwanda aliyetoweka na kufariki, nataka kukuhakikishia kwamba tunachukua kila hatua sio tu katika eneo la Rufiji bali pia maeneo mengine ya Tanzania ili kuhakikisha kuwa watu wetu wako salama sio tu waandishi , bali pia Polisi na raia wa kawaida


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad