Ujumbe wa Kenyatta kwa JPM Kuhusu Jaguar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ujumbe wa Kenyatta kwa JPM kuhusu Jaguar
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemtumia ujumbe maalumu Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli unaoelezea msimamo wa Serikali yake kuhusu kukerwa na matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa jimbo la Starehe, Charles Njagua Kanyi maarufu kwa jina la Jaguar.

Ujumbe huo wa maandishi umewasilishwa na Balozi wa Kenya nchini, Dany Kazungu na kupokelewa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli, ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar Es Salaam. 

Akipokea taarifa hiyo Waziri Mkuu amesema Watanzania wamefurahishwa na hatua mbalimbali zilizochukulia na Serikali ya Kenya dhidi ya mbunge huyo zinazodhihirisha kwamba matamshi hayo hayakuwa msimamo wa Serikali ya Kenya wala wananchi wake bali ulikuwa ni msimamo  binafsi wa mbunge huyo.

"Uhusiano kati ya Kenya na Tanzania ni wa karibu mno na wa kindugu kwani kuna baadhi ya makabila yapo katika nchi mbili hizi kama vile Wamasai na Wakurya na  Wajaluo  hivyo ushirikiano katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kabiashara na ya kijamii haukwepeki." amesema Waziri Mkuu

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi na wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kujiepusha na kauli zenye viashiria vya  kujenga chuki, uhasama na migongano miongoni mwa wananchi kwani kauli hizo zisipodhibitiwa mapema zinaweza kusabisha hofu na kutokuelewana miongoni mwao.

"Mambo yetu yote katika nchi za Afrika ya Mashariki  hasa ya biashara na ya  kiuchumi kwa ujumla yataenda vizuri endapo  tutalinda na kudumisha amani, bila amani tutaogopana na tutashindwa kabisa  kushirikiana", amesisitiza Mheshimiwa Majaliwa.

Julai 24, 2019 kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa kipande cha video kikimuonesha Mbunge Jaguar, akitoa kauli ambazo zilitafsiriwa zililenga kuleta ubaguzi baina ya wananchi wa Kenya na Tanzania lakini baadaye mwenyewe alikanusha kuwa hakuwalenga watanzania bali walikuwa watu wenye asili ya China.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad