VIDEO: Ozil, Kolasinac Wanusurika Kuchomwa Kisu, Kolasinac Aibuka Shujaa Baada ya Kupigana Nao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wachezaji wawili wa timu ya Arsenal ya nchini England Sead Kolasinac na Mesut Ozil akiwa na mkewe, wamevamiwa jana kaskazini mwa Jiji la London na watu wawili waliokuwa na visu katika kile kilichoonekana kuwa tukio la ujambazi. Hata hivyo shukrani za pekee ziende kwa Kolasinac ambaye alipambana kuwaokoa jahazi.

Ozil alikuwa kwenye gari lake jeusi aina ya Mercedez kwenye makazi ya Kolasinac wakati watekaji hao walipojaribu kutekeleza jaribio hilo.


Katika picha ya video inayosambaa kupitia mtandao, Kolasinac anaonekana akipambana na wahalifu hao huku Ozil na mkewe wakiwa wamebaki kwenye gari.

Baadaye Kolasinac aliingia kwenye gari huku, wahalifu hao wakiwa bado wanaendelea kuwafuata kwa nyuma. Hata hivyo taarifa zinasema kuwa baadaye wahalifu hao waliondoka baada ya Kolasinac kuondoa gari kwa nguvu kwa nia ya kuwagonga.

Mpaka sasa, watu kadhaa wanashikiliwa kutokana na tukio hilo ambalo bado lipo chini ya uchunguzi. VIDEO:
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad