Wafahamu Makocha Waliotimuliwa Kazi Baada ya Michuano ya Afcon Kumalizika Nchini Misri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Herve Renard anajiuzulu kama kocha mkuu wa Morocco baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika kashindani ya kombe la mataifa ya Afrika. Morocco ni mojawapo wa timu zilizopigiwa upatu kabla ya kuanza kwa mahsindano hayo Misri 2019 lakini ilishindwa kupitia mikwaju ya penalti na Benin katika timu 16 za mwisho.

Renard, raia wa Ufaransa amewahi kushinda mataji mawili ya Afcon na Zambia (2012) na Ivory Coast mnamo 2015, alikiongoza kikosi cha Morocco tangu Februari 2016.

“Umwadia wasaa wa mimi kuufunga ukurasa huu mrefu na mzuri katika maisha yangu,” amesema Renard mwenye miaka 50.

Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii, Renard amesema “Ni uamuzi usioweza kuepukika ulichukuliwa hata kabl aya kuanza mashindano ya Afcon 2019.

“Nilichukua uamuzi huu- bila shaka – baada ya kutafakari kwa makini. kwahivyo siwezi kuugeuza.”

Renard aliitoa Morocco kutoka nafasi ya 81 katika orodha ya Fifa duniani hadi katika nafasi ya 47.

Hatahivyo Renard siyo kocha wa kwanza kuondoka au kuondolewa kutokana na matokeo duni katika mashindano hayo yaliokamilika mwaka huu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mapemamwezi Julai limetangaza kusitisha mkataba na kocha Emmanuel Amunike.

Taarifa fupi iliyotolewa na TFF inadai kuwa Amunike amekubaliana na TFF kusitisha mkataba huo.

“Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019,” ilisema taarifa ya TFF.

Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018.

Atabakia kwenye historia ya mpira Tanzania kwa kuingoza nchi hiyo kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya miaka 39.

Kabla ya hapo alinyanyua Kombe la Dunia 2015 akiwa kocha wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 Nigeria.

Kocha huyo ni winga wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Barcelona.

Hata hivyo, Amunike amekuwa akilaumiwa na baadhi ya mashabiki kwa namna anavyoteua wachezaji na kupanga kikosi.

Tanzania ilitolewa katika mashindano ya Afcon baada ya kupoteza michezo yote ya makundi.


Sebastien Desabre aliachia nafasi ya ukocha wa Uganda kwa ridhaa yake baada ya timu yake kuiaga michuano ya AFCON.

Uganda ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Senegal jijini Cairo katika mchezo wa hatua ya 16 bora.

Shirikisho la soka Uganda, Fufa limesema Desabre ameondoka huku akiwa amebakiwa na miezi mitano kumaliza mkataba wake.

”FUFA inatoa shukrani kwa mchango wa Desabre kwenye maendeleo ya soka la Uganda na timu ya Uganda Cranes” Ilisema taarifa hiyo.

Desabre, 42 amekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uganda tangu aliposaini mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo mwezi Desemba mwaka 2017.

Kabla ya Cranes kupoteza mbele ya Senegal, wachezaji waligomea mazoezi, mzozo uliokuwa kati ya wachezaji na Fufa kuhusu malipo.

Misri yamng’oa Javier Aguirre baada ya hatua ya 16 bora
Aguirre was only appointed last August on a four-year dealHaki miliki ya pichaAFP
Misri imemng’oa Javier Aguirre baada ya wenyeji kufungwa katika hatua ya 16 bora katika mashindano hayo ya Afcon.

Pharaohs kama inavyojiita timu hiyo ya taifa walipigiwa upatu pia kabla ya kuanza kwa mashindano hayo lakini ilifungwa 1-0 mjini Cairo baada ya bao alilosukuma Thembinkosi Lorch wa Afrika kusini kunako dakika ya 85.

Rais wa shirikisho la soka Misri Hany Abo Rida pia alijiuzulu akisema lilikuwa ni ‘jukumu la kimaadili’.

Aguirre, ambaye ni raia wa mexico mwenye umri wa miaka 60, alijiunga na kikosi hicho cha Misri mnamo 2018,na kumrithi Hector Cuper, aliyeondoka baada ya kushindwa katika kombe la dunia.

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Uholanzi Clarence Seedorf alitimuliwa kama kocha wa Cameroon baada ya upande wake kushindwa kulitetea taji la Afcon mwaka huu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 43, alikuwa mkufunzi kwa chini ya mwaka mmoja.

Naibu wake Patrick Kluivert, pia ameondoshwa.

Seedorf alisema angefurahia kuendelea na alihisi kuwa kikosi chake kimeonyesha matumaini

Alisaini mkataba wa miaka minne kukiongoza kikosi cha Indomitable Lions mnamo Agosti 2018.

Lakini taarifa ilithibitisha kwamba ” shirikisho la soka Cameroon kwa mujibu wa vifungu katika mikataba yao imeamua kusitisha mkataba wa Seedorf na Kluivert”.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad