Tanasha ataja idadi ya ‘wapenzi’ wake kabla ya kukutana na DiamondDar es Salaam. Tanasha Donna, mpenzi wa Diamond Platinumz  amesema hawezi kufuatilia wapenzi  wa zamani wa msanii  huyo wa Bongo Fleva kwa sababu kabla ya kuwa naye, alikuwa na uhusiano na wanaume watatu.


Kauli ya Tanasha imekuja siku kadhaa baada ya mpenzi wa zamani wa Diamond,  Zarina Hassan‘Zarithebosslady’ kumtakia kheri, kumtahadharisha ajipange kulea mtoto wake kutokana na aina ya baba aliyezaa naye ambaye ni Diamond. 

“Siwezi kumlaumu kwa mahusiano yaliyopita kwani hata mimi kabla ya Diamond nilikuwa na wapenzi watatu, siyo shida na yeye akiwa nao, ”amesema mkali huyo wa wimbo 'Nah Easy'.


Amefafanua kuwa mpaka sasa hajaona tatizo lolote kwenye uhusiano wao, ndio maana hashughulishwi na mahusiano yaliyopita ya Diamond. 

“Siwezi kumtilisha shaka kwa vitu alivyowafanyia wengine, namuangalia na kumpima mtu ninapokuwa naye binafsi, akifanya kitu tofauti na makubaliano yetu sawa, lakini sio kwa sababu aliwahi kuwafanyia wengine na mimi nipate hofu, ”amesema.


Mapema 2019,  Diamond aliwahi kummwagia sifa mrembo huyo kwamba ni mwanamke anayejielewa, anafanya vitu vyake kwa mpangilio, na hana muda wa kurushiana vijembe mtandaoni.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Tanasha ataja idadi ya ‘wapenzi’ wake kabla ya kukutana na Diamond Tanasha ataja idadi ya ‘wapenzi’ wake kabla ya kukutana na Diamond Reviewed by Udaku Special on August 20, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.