Maalim Seif Akamatwa na Polisi


Chama cha ACT- Wazalendo kimethibitisha kukamatwa na Jeshi la polisi  kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho akiwemo mshauri mkuu, Maalim Seif, Katibu wa kamati ya uadilifu, Mbarala Maharagande, wakati wa harakati za uzinduzi wa matawi katika Kata ya Azimio Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.

Hayo yamethibitishwa na Katibu Msaidizi wa kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT-Wazalendo, Seif Suleimani ambapo amesema kuwa Jeshi la polisi lilifika na kumzuia Mshauri Mkuu Maalim Seif kufanya uzinduzi.

”Jeshi la polisi kutuzuia kufanya shughuli zetu kuu za msingi za kisiasa ni kutuingilia na kuingilia uhuru wetu wa chama cha siasa, na tunalitaka jeshi la polisi mara moja liache kutuingilia katika kufanya shughuli zetu za kisiasa,”amesema Seif.

Aidha, kiongozi huyo amesema chama hicho kinafanya shughuli ya uzinduzi wa matawi mapya ikiwa ni hatua ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa kama vyama vingine vya siasa vinavyofanya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Maalim Seif Akamatwa na Polisi Maalim Seif Akamatwa na Polisi Reviewed by Udaku Special on August 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.