Rosa Ree Amkana Msanii wa Kenya Timmy Dat

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanadada anayefanya vizuri kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Rosa Ree 'Goddess Of Rap' amefunguka kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na msanii Timmy Tdat wa Kenya.


Rapa huyo wa kike amesema hayo kupitia EATV/Radio Digital baadaya kuulizwa kuhusu uhusiano wake na Timmy Tdat, ambapo amesema,

“Timmy Tdat hajambo ila shemeji yenu mimi simfahamu, ni kazi kama mnavyoweza kuona hakuna hata siku moja mkatuona tuko pamoja kiundani, kingine ni washkaji sana, mimi nina mahusiano mengi ya M\Mungu, familia yangu, kazi na sina muda wa kuwa na mahusiano mengine ya aina yoyote”

Wawili hao wamekuwa wakitajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ya siri kutokana na ukaribu walikokuwa nao, muda mwingi walionekana pamoja, kupiga picha na pia kusafiri pamoja.

Rosa Ree na Timmy Tdat walianza kuonekana wakiwa pamoja mwanzoni mwa mwaka huu wakiwa nchini Kenya na Tanzania. Pia aliwahi kusema bado hajapata mwanaume wa kuwa naye.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad