Shiboub Apata Dawa ya Do Songo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KIUNGO Msudan wa Simba, Sharaf Shiboub amefunguka kuwa dawa pekee ya kuwafunga wapinzani wao, UD do Songo kwenye mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa ni kuona wanapata sapoti kubwa ya mashabiki wao kwenda kuwashangilia.

Kiungo huyo keshokutwa Jumapili atakuwa mmoja ya wachezaji ambao watakuwa na kibarua cha kupambana na Do Songo kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa suluhu nchini Msumbiji.

Katika mchezo huo Simba wanahitaji ushindi wa namna yoyote ili kusonga mbele katika hatua inayofuata. Kiungo huyo amesema kuwa ana imani kubwa ya kushinda kwenye mechi hiyo lakini morali yao itaongezeka zaidi mashabiki wao watakapokuwa wengi uwanjani hapo kwa ajili ya kuwashangilia.

“Tuna matumaini makubwa ya kushinda mechi hii kwa sababu tuko nyumbani na tumejiandaa vizuri, lakini naona kabisa kama mashabiki wetu wakiwa wengi itakuwa vizuri zaidi.

“Wakiwepo mashabiki wengi kwenye mechi hiyo kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Azam basi naamini kabisa litakuwa jambo zuri kwetu kuweza kushinda mchezo huo,” alisema Msudan huyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad