Waandishi Waifuata Burundi Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MSAFARA wa watu 40 utakaojumuisha Waandishi wa Habari za michezo Tanzania na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unatarajiwa kuondoka Tanzania, leo Jumamosi kuelekea Burundi kuisapoti Taifa Stars.

Katika msafara huo, waandishi watakuwa 35 na viongozi wa TFF watano ambapo wanakwenda kuisapoti Taifa Stars itakapocheza na Burundi, Jumatano ijayo mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.

Akizungumza na Championi Jumamosi, msemaji wa waandishi watakaosafiri, Ally Kamwe alisema kuwa maandalizi ya safari hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa kwa kuwa wanatarajia kuondoka leo nchini hapa kuelekea Burundi kwa ajili ya mchezo huo.

“Kiukweli maandaalizi ya safari yetu yamekamilika kesho (leo Jumamosi) ndiyo tuanza safari yetu ya kuelekea Burundi kwa msafara wa waandishi 35 na maofisa watano kutoka shirikisho.

“Tunatarajia kupumzika Dodoma halafu baada ya hapo tutapumzika Kahama ambapo hapo tutafanya shughuli kubwa ya uhamasishaji ikiwemo kupita katika baadhi ya redio na tutaungana na Watanzania wengine ambao wanatarajia kwenda huko kuipa sapoti timu yetu na Burundi tunatarajia kuingia siku ya Jumatatu jioni,” alisema Kamwe.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad