Yajue Madhara ya Kuingiza Vitu Ukeni au Kuuosha Kwa Sabuni

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Hivi karibuni kumekua na malalamiko mengi toka kwa wasichana kutopata ujauzito na wengine kutofurahia pale wanaposhiriki tendo la ndoa.

Wanawake wengi hasa wenye umri kati ya miaka 18-45 wamekua wakikumbwa na matatizo mbalimbali ya uzazi bila kujua kwamba kwa namna moja ama nyingine wao wenyewe ndio chanzo cha matatizo hayo.

Leo nimekuja na taarifa na tahadhari zilizotolewa na madaktari wakubwa nchini marekani ambao wameeleza mambo gani ya kuzingatia na kutothubutu hata kujaribu kwa kulinda afya ya uzazi na kutoharibu uke wako.

Mtaalamu wa Constance Young Daktari na profesa katika chuo cha Columbia University anatueleza mambo ya kuzingatia kutoharibu uke wako.

1.VAGINAL DOUCHING

Hii ile tabia ya kuosha sehemu za ndani ya uke kwa kutumia viosheo maalumu vinavyopatikana madukani au supermarket mbali mbali, Hapana hii ni tofauti na ule unawaji wa kawaida au uoshaji wa kawaida unapokwenda kuoga, haijakatazwa kuosha uke wako kwa maji ya uvuguvugu kwa kuwa hiyo ni salama na haina matatizo kiafya.

Vagina douching ni kule kutumia sabuni za maji au maji maalumu ambayo yanakua yamechanganywa na iodine,vinegar na magadi na kuyaingiza ndani ya uke, hii ni hatari kwa afya ya uke wako.

Njia bora ya kujisafisha ni kutumia maji ya uvuguvugu pale unapooga kwa kusafisha sehemu za nje na sio ndani ya uke kwakua inaelezwa kwamba uke hua unajisafisha wenyewe kwani hutoa kitu kinachoitwa mucous ambayo ina control damu na uchafu mbali mbali ndani ya uke.

2. INSERTING UFOs
Najua unafahamu kipi kinatakiwa kiingie na kipi kisiingie kwenye njia yako ya uzazi[ukeni],vidole,uume, na vifaa vya hedhi sio tatizo kiafya ila kumekua na tabia kwa baadhi ya wanawake kutumia ndizi na vitu vinavyofanana na hivo katika kile kinacho aminika kujiridhisha pale anapokua mbali na mwenzi wake.

Kama hujawahi kufanya tafadhari usijaribu na kama unafanya acha mara moja vitu hivi husababisha vaginal irritation ni maumivu katika uke na michubuko ambayo itakufanya usifurahie tendo la ndoa.

3.SELF MEDICATING
Dk. Dardik ameeleza kuwa tabia ya kujitibu bila kuwaona madakta wa matatizo ya wanawake si jambo nzuri kwa kuwa imesababisha matatizo makubwa kwa wanawake wengi ameeleza kuwa kuna wanawake wanatumia vitunguu swaumu, limao na wengine hata sabuni bila ya kufuta utaratibu na ushauri wa daktari.

Uke umejumuisha bakteria wabaya na wazuri wote hao wanakazi maalumu ya kufanya usawa wa homoni ukeni, matumizi ya madawa makali husababisha uwepo wa bakteria wabaya na hatimaye mwanamke anaweza kuona siku zake za hedhi haziendi sawa na wengine kutokwa damu nyingi na maumivu makali wanapokuwa katika mzunguko.

4.VAGINAL STEAMING

Hiki ni kitendo cha kujifukiza kwa marashi, kumekua kiaminika na baadhi ya matabibu wa asili kutokea nchi za uchina, korea na japani ambao wameambukiza hadi mataifa kama Marekani na Uingereza tendo hili huitwa vaginal steaming huchukuliwa marashi yanaitwa VAGI-STEAM na mwanamke hukaa juu ya kiti ambacho chini yake kuna bakuli yenye maji yamoto na mvuke huo huenda moja kwa moja kwenye sehemu za uke.

Jambo hili hufanywa kwa nia ya kusafisha uke lakini imepigwa vita na madaktari wakieleza kwamba si sahihi kwani huwaondoa baadhi ya bakteria wanaotakiwa katika kurekebisha mfumo wa homoni na kusababisha madhara.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad