9/20/2019

Alikiba – Ni kweli mke wangu nilimrudisha kwao, wasipende kuingilia maisha ya watu


Msanii wa muziki nchini, Ali Kiba amefunguka kuhusu maneno ambayo yamekuwa yakisambaa mtandaoni kuhusu yeye kumtalaka mkewe na suala la mke wake kujihusisha na ushirikina.

King akizungumza katika moja ya chombo cha habari hapa nchini, Clouds Radio amesema kuwa katika mambo yote yaliyoongelewa mtandaoni kuhusu mke wake ni asilimia moja tu yana ukweli huku asilimia 99 yakiwa si ya kweli.

Japokuwa amekiri kuwa yeye na mke wake Bi Amina wamekuwa na ugomvi wa hapa na pale jambo ambalo ni kawaida kwenye maisha ya familia hasa kwa wanandoa.

Kiba amesema kufuatia uzushi mwingi unaoendelea mitandaoni umekuwa ukimsumbua hivyo ameamua kuja kuongelea jambo hili ili kuweka sawa uzushi ambao umesambaa hivi karibuni kwani anaamini kuwa huenda uzushi huo ukawa ndio chanzo namba moja kuvunja ndoa yake.

”Ni kweli mimi na mke wangu tunugomvi wa hapa na pale ambayo ni kawaida kwenye familia na niliweza kumrudisha kwao mimi mwenyewe na si kumrudisha kwamba tuligombana wala nini nilikuwa na safari ya kwenda Europe nilimpeleka kule, lakini niliona kwa nini nisimrudishe kazini aendelee kufanya kazi wakati mimi nikiwa huko, niliona niendelee kumuacha afanye kazi maana yeye amesoma kichwa chake kitalala” amesema Alikiba.

Aidha, ameshauri watu kutoendeshwa au kufuatisha mambo katika mitandao ya kijamii na si jambo la baraka kushabikia watu wanapogombana, pia ameshauri watu kutoingilia maisha binafsi ya watu hasa ya ndoa kwani kuna utofauti mkubwa sana katika maisha ya uchumba na maisha ya ndoa.

Amemalizia kwa kusema kuwa yeye na mke wake wapo sawa na hajawahi kumpa talaka japokuwa dini yake inamruhusu kumpa talaka pale anapokuwa amemkosea na kuoa mke mwingine siku inayofuata, amesema kuwa yeye na mke wake wapo fresh hata sasa wanafanya mazungumzo kama kawaida.

Ameomba watu wajiheshimu kwani amesema heshima ni kama kufunga mlango na kuondoka wasipende kuingilia maisha ya watu hasa ya ndoa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

2 comments:

  1. Bora umeamua kuongea mwenyewe maanabwambeya walisema eti umempa mkeo talaka tatu, kuna watu hawapendi kuona wenzao wanaishi kwa amani na upendo.

    ReplyDelete
  2. Bora umeongea ukweli, nyinyi si malaika muishi bila kugombana.

    ReplyDelete

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger