Fatma Karume amburuza mahakamani Mwanaharakati Cyprian Musiba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amemshtaki Cyprian Musiba katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa madai ya kukashifiwa na mwanaharakati huyo.

Akizungumzia shtaka hilo, Fatma Karume amedai kuwa wanatakiwa kufika katika mahakamani Oktoba 3 mwaka huu, Kwa ajili ya kutajwa kwa kesi hiyo Na. 39 ya mwaka 2019.

“Ninamshtaki kwa kunikashfu kwa kusema kwamba eti nimetiwa mimba na muuza unga, na kwamba sina staha, mimi nina mume na watoto, sasa siwezi kukubali ujinga huu,“ameeleza Fatma kwenye mahojiano yake na gazeti la Nipashe.

Fatma ambaye pia ni wakili wa kujitegemea, anaungana na Waziri wa zamani Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kufungua mashtaka kwa madai ya kushushwa hadhi na Musiba.

Mwanaharakati huyo ambaye amekuwa akijipambanua kuitetea serikali, amekuwa akiingia katika migogoro na watu mbalimbali ikiwamo hivi karibuni kuingia katika vita ya maneno na Waziri wa Mambo ya Ndani na Nchi, Kangi Lugola, baada ya waziri huyo kumtaka kutofautisha harakati zake na serikali
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad