Haya Ndio Anayoyapenda Mume Wangu na Kuiharibu Ndoa Yangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndugu zangu,
Nilishawai kuwaambia hali ngumu ya mapenzi ninayoipitia ndani ya miaka miwili,kwa kifupi ni kuwa mwanaume unalalanae miezi 2 hajakugusa, ukimgusa anasema amechoka.

Juzi nilikuwa napitia Fb yake nimekuta amewa add wadada wa 4 hivi tofauti na katika wadada hao wote ni ambao mtu anaejiheshimu na mwenye busara hawezi kuwa add, ni watu wasio na maadili mema, picha zao zimekaa kikujiuza, na ata ukiangalia friends wao hao kina dada ni wanaume zaidi ya 600.

Wanawake unaweza kuta wa4 tu, mr. uwa anasafiri sana kikazi anaenda jiji flani hapahapa TZ na hao aliowa add wanapatikana jiji hilohilo nikiangalia profile zao, naanza kuamini kuwa hii hali ngumu ya mapenzi ninayopitia anaisababisha yeye kwa makusudi na wala sio shetani bali anaudekeza moyo wake unachoona.

Hivohivo, sijamuuliza na sitomuuliza naona tabu kumuuliza maana nishalalamika sana lakini sioni mabadiliko, sio wanaume wote wanaosafiri kikazi wanaendea kazi wengine wanaendea ufuska tu.Nilijaribu kwenda katika fb page nikaingiza namba yake nimekuta ana account nyingine nayo haieleweki.

Kaiita kama majina kama vile (Zanzibarbongo) sio jina halisi, hapa mnielewe namaanisha hivi namba ya simu ukiisajili katika kufungulia account ya fb inaonesha hiyo account, so baada ya kuweka namba yake nimekutana na hiyo account it means kwamba ya kwake, wakati huohuo ana account ambayo inafahamika,

Najiuliza anatafuta nini? Mke wake mie msichana tu, najimudu, nafanya kazi mzuri, nina umbo zuri, na kazi zote nifanyazo lazima nihakikishe napika chakula cha usiku kwa mkono wangu, na mengine yote ya kumfanyia mume namfanyia, jamani huyu mwanaume asieridhika na alichonacho anatafuta nini?

All in all nimechoka na hii hali na siku zinavoenda mapenzi yanaisha kabisa kwake.

Nifanye nini ndugu zangu?
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kawaida ya mapenzi huwa na 'stage' 3,hatua ya kwanza ni pale mnapoanzisha uhusiano wenu,kila mmoja wenu anataka awe karibu na mwenziwake muda wote,lkn sababu ya majukumu ya utafutaji wa rizki ya kila siku,basi hujikuta mnakutana mmalizapo majukumu yenu ya kila siku,,,,hapa penzi huwa 'shatashata',sasa tunakwenda hatua ya pili, hii hatua ya PILI hii hatua ndo ina utata na ndo hatua ngumu sana,na hii ndo hatua unayokutana nayo mtoa mada.kumbuka hatua hii penzi huchujuka kati ya mmoja wenu kama sio wote wawili,kuna kuchokana,mazoea ndo yanafanya muwe pamoja na kama wote mnakuwa mmechokana ni rahisi sana kama ni uhusiano au ndoa kuvunjika coz wotepenzi 'limechujuka'.ila kama mmoja bado ana moto ule ule wa mahaba niue,walao penzi linaweza kuendelea ikiwa anaependa atagundua kuwa mwenzie hamtaki au hampendi tena,hapa muhusika apae ndo bado anapenda inabidi awe mbunifu na mtundu wa kuleta mageuzi au mabadiliko mapya katika penzi ili yule aliye kuwa hapendi apate kurudi kwenye mstari,hapa asilimia 90 penzi litarudi na hatua ya tatu na mwisho utegemee na wewe uliyechokwa kipndi kile cha pili nawe pia hatua hii ya tatu utachoka,hapa napo upande wa pili lazima ugundue na ubadilishe upepo,mkivuka hatua hii mtakaa pamoja katika ndoa au mahusiano mpaka mtakapoiacha dunia,,,,mtoa mada fatilia hizi steps in deep utapata jibu ikiwa kweli bado unamhitaji mumeo,pasipo ugomvi wala jazba,,,,,,masalaam.

    ReplyDelete
  2. kwa nini usitafute taraka?

    ReplyDelete
  3. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    ReplyDelete

Top Post Ad