Kijana Adakwa akiwa na sare za Jeshi la Polisi na mali za wizi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Kelvin Manyusi (32) fundi umeme, mkazi wa Teku Jijini Mbeya akiwa na sare za Jeshi la Polisi ambazo ni TT 2 kitengo cha FFU, koti la mvua rangi nyeusi pamoja na mkanda wa filimbi ambavyo ni mali za Jeshi la Polisi Tanzania.

Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 20, 2019 saa 15:30 alasiri katika msako uliofanyika huko Mtaa wa Ngosi, Kata ya Mwakibete, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya.

Pia mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na vifaa vya kuvunjia ambavyo ni panga, bisibisi pamoja na tindo. Aidha mtuhumiwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na mali mbalimbali zidhaniwazo kuwa za wizi ambazo ni

1.“TV” 2 aina ya “Samsung” nchi 32, “Aborder” nchi 32,
2.“System Case” mbili aina ya “Dell na Hp”,
3.“Keyboard” 1 aina ya “Hp”,
4.“Receiver” tatu za vinga’muzi vya “Dstv”, Azam na “Startime”,
5.Speaker” mbili za “Seapiano” na “Topsonise”,
6.Simu za Mkononi 9 kati yake “Smartphone” tatu na sita za kawaida 6,
“External” 4,
7.Kamera moja aina ya “Ricoh”,
8.“Remote control” 14,
9.“Switch ya Internet” 1,
10.“Dryer” mbili moja ya mkono ndogo na kubwa,
11.Jiko la umeme 1,
12.Amplifier na Equalizer 1 aina ya metal,
13.Twitter 7,
14.mouse 1,
15.Rasta bunda 7 za kusukia nywele bandia,
16.Uzi bunda mbili za kushonea,
17.Mashine ya Blenda nyeupe ,
18.Saa 3,
19.Deki 1 aina ya LG,
20.Mitungi 2 ya Gesi aina ya Oryx,
21.Jiko la Gesi 1 la plate mbili.
22.Upelelezi unaendelea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad