9/17/2019

Madam Rita ajivunia miaka 10 ya BSS

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Benchmark Productions na Jaji Mkuu wa shindano la kusaka vipaji Bongo Star Search (BSS), Rita Paulsen ana furaha na anajivunia kufanikiwa kuvumbua vipaji vya kuimba vya vijana mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo , wakati wakitangaza msimu mpya wa shindano hilo litakaloanzia mkoani Arusha, amesema BSS imefanikiwa kuwapa nafasi vijana hao wa kitanzania kuendeleza maisha ya kimuziki na wengine kufanikiwa nje ya muziki pia.

“Kwa sababu ni ‘anniversary’ ya miaka 10 ya Bongo Star Search, najivunia vipaji ambavyo tumevileta mbele ya Watanzania na kufanikiwa kueneleza vipaji vyao nje ya muziki."

“Kuhusu ujio wa msimu wa 10 huku akitaja ongezeko la mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa shindano hilo, habari njema sana kwa Watanzania ni kwamba tumeongeza idadi ya mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa BSS mwaka huu ni Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam,” amesema.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger