9/14/2019

Rais Ramaphosa azomewa Zimbabwe, aomba msamaha

 Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amewaomba waafrika msamaha pamoja na kuonesha kujuta kwake, kufuatia mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni yaliyotokea siku za hivi karibuni nchini humo na amewakaribisha raia wa mataifa mengine kwenda huko akisema hali hiyo haitotokea tena.


Akizungumza leo Septemba 14, 2019 wakati wa Shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe yaliyofanyika katika uwanja wa Mpira wa Harare nchini humo, Rais Ramaphosa amesema kuwa kilichotokea nchini kwake ni kinyume na taratibu za makubaliano kwa viongozi wa nchi hizo.

Rais Ramaphosa alionyesha masikitiko yake baada ya wazimbabwe kuanza kupiga mayowe, punde tu alipokaribishwa kutoa hotuba yake fupi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa Tanzania inahuzunika kama ambavyo wao wanahuzunika kwa kupoteza kiongozi shujaa na mahiri.

Mwili wa Mugabe utazikwa kijiji alichozaliwa cha Kutama kilichopo katika jimbo la magharibi la Mashonaland yapata kilomita 80 au maili 50 magharibi mwa mji mkuu Harare.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger