UPDATE: Mawakili wapinga ndege ya Air Tanzania kuzuiwa Afrika Kusini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dar es Salaam. Jopo ya wanasheria waliopelekwa na Tanzania kupinga amri ya kushikiliwa kwa ndege ya Air Tanzania wameiambia mahakama ya Gauteng, Afrika Kusini kwamba amri ya kushikiliwa ndege hiyo ilitolewa kimakosa.

“Tumeonyesha kwamba amri ya kuishikilia ndege ya  Air Tanzania aina ya airbus A220-300 ilitolewa kimakosa dhidi ya Serikali, kwa hiyo tumetaka iondolewe,” wakili  Ngaukaitobi aliiambia mahakama.

Wakili Roger Wakefied anayemwakilisha mkulima Hermanus Steyn amesisitiza kuwa kuna kesi ya msingi ya kujibu na ameitaka mahakama hiyo kuangalia vigezo vya madai hayo na kuvitendea haki.

Kwa mujibu wa Wakefield hatua ya kwanza ya vigezo vya kesi hiyo vimeshathibitishwa.

Ndege hiyo ilishikiliwa Agosti 23, 2019 nchini humo kutokana na mvutano wa kisheria uliodumu kwa miongo kadhaa kati ya Serikali ya Tanzania na mkulima  Hermanus Steyn.

Mali za Steyn ikiwemo kampuni ya mbegu ya Rift Valley Seed Company Limited na mali nyinginezo zilitaifishwa na Serikali ya Tanzania Januari 1982. Amekuwa akiidai Serikali Sh373 milioni.


Hata hivyo, Julai 9, 2010 Jaji mstaafu Josephat Mackanja wa mahakama kuu alimpa Steyn tuzo ya Dola za Kimarekani 36,375,672.81.

Kuna ushahidi kuwa baada ya kutolewa kwa tuzo na Mahakama hiyo kulikuwa na makubaliano kati ya pande mbili yaliyoishusha hadi kufikia Dola 30 milioni na Serikali ya Tanzania ililipa kiasi kikubwa cha deni hilo kupunguza madai hayo.

Akizungumza na gazeti la Daily News, Wakili mkuu wa Serikali, Ally Possi amesema timu ya mawakili wanane kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali watapambana kwenye kesi hiyo iliyotajwa Agosti 21, 2019  ambayo hati ya dharura iliwekwa na kampuni ya mawakili ya Werksman’s Attorneys ikitaka ndege yoyote ya ATCL ili kufanikisha malipo ya tuzo hiyo.

 Mwananchi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad