9/21/2019

Waziri ataka wapenzi wa jinsia moja kukamatwa Zanzibar


Naibu waziri wa mambo ya ndani kisiwani Zanzibar Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza jeshi la polisi visiwani humo kuwakamata wanaoendesha maswala ya Ushoga na unyanyasaji wa kijinsia.

Amesema kwamba swala hilo ni kinyume na misingi ya dini zote ambazo Watanzania na Wazanzibare wanaamini.

''Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya watoto wa kiume wameharibiwa na baadaye tunaona ongezeko la wimbi la vijana wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja'', alisema.

''Natoa wito kwa jeshi la polisi kuhakikisha kwamba wale wote ambao wamekuwa na desturi ama utamaduni wa kushiriki ama kuhamasisha vitendo hivi vibovu na viovu katika nchi yetu kuhakikisha kuwa wanachukuliwa hatua kali'', aliongezea.

Hakimiliki ya Picha @WizaraMNN@WIZARAMNN
Amesema kwamba mbali na vijana kujihusisha katika vitendo hivyo pia wamekuwa wakihusika pakubwa katika ulanguzi wa mihadarati katika maeneo hayo.

Amesema kwamba visiwa hivyo vinakumbwa na changamoto hizo ambazo anadai kwamba zinachafua taswira na heshima ya visiwa hivyo viwii mbali na kusababisha mmomonyoko wa maadili katika visiwa hivyo viwili.

Hatahivyo amesisitiza kwamba ili kukomesha tabia kama hizo ni sharti wananchi wote kuwa kitu kimoja katika kuyakemea na kuyazuilia maovu hayo yasiendelee.

Tayari shirika moja linaloshughulikia kuwabadilisha tabia wapenzi wa Jinsia moja mbali na kuwapa msaada wa kiafya wanaume hao limebuniwa .

Shirika la IYAHIZA linahusika na mapambano ya virusi vya ukimwi kwa vijana visiwani Zanzibar na miongoni mwa miradi wanayoshugulikia ni kuyasaidia makundi maalum, ikiwemo wanaume wanaojihusisha na Mapenzi ya Jinsia Moja.

Mbinu mbalimbali hutumiwa, kwanza hufuatwa kisha kupewa ushauri na kupimwa ikiwa wana maambukizi ya magonjwa yoyote ikiwemo virusi vya Ukimwi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger