Asilimia 91 ya Mashabiki Manchester United Wamtaka Mwarabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

UTAFITI wa mitandaoni umeonyesha kuwa asilimia 91 ya mashabiki wa Manchester United wanataka bilionea wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman awe mmiliki wa timu hiyo achukue nafasi ya Familia ya Glazer.



Klabu hiyo ilitajwa kuwa inataka kununuliwa na bilionea huyo Mwarabu kwa pauni bilioni 3 lakini maombi yakakataliwa.

Mashabiki wa United wanaamini familia ya Glazer imeshindwa kuiongoza klabu hiyo na hivyo suluhisho pekee ni Bin Salman kuinunua United.



Kura zimepigwa zaidi ya 8,000 ambapo zimeonyesha kuwa ni muda wa mabadiliko.

Kumekuwa na taarifa kuwa mmoja wa wamiliki wa United, Kevin Glazer anataka kuuza hisa zake za asilimia 13.



Pamoja na mipango hiyo ya Kevin kutaka kuuza hisa zake lakini bado kutatakiwa ushawishi mwingine utoke kwenye familia yake ambapo kwa pamoja wanamiliki hisa za kuimiliki United ambao ni Avram, Joel, Bryan, Edward na Darcie Glazer.



Familia hiyo ya Kimarekani iliinunua United kwa pauni 790m miaka 14 iliyopita lakini kumekuwa na madeni mengi ambapo mashabiki wanaamini yamechangia timu yao kutokuwa sawa kiuchumi
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad