Askari Polisi mbaroni kwa tuhuma za Rushwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa  (TAKUKURU) mkoani Kagera inamshikilia  askali wa jeshi la wananchi Tanzania mwenye cheo cha Koplo(Corporal) aitwaye Nyambita Makayaga Magoma kwa kuomba rushwa.

Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa Takukuru mkoa John Joseph amesema kuwa askali huyo anashikiliwa kwa kosa la kuomba rushwa kwa mkazi mmoja wa wilaya ya Biharamulo kijiji cha Nemba Tsh. 3,000,000 kwa kosa la kuingiza ng’ombe katika hifadhi ya taifa(Biharamulo forest reserve.

Pamoja na hayo uchunguzi wa Takukuru ulibaini kuwa licha ya askali huyo kuomba kiasi hicho cha fedha Askali huyo alishikiliwa  mifugo hiyo mpaka  alipopatiwa jumla ya Tsh.800,000  na kisha kumwachia mwananchi huyo ambaye alilazimika kutoa taarifa hizo Takukuru.

Aidha ameongeza kuwa taasisi hiyo pia inamshikilia Koplo  (Coplo) Nassoro Maulidy Mirambo kutoka kituo cha Runazi kwa kushilikiana na Bw. Asaph Manya Manya ambaye ni mwajiriwa katika Harmashauli ya wilaya ya Biharamulo idara ya misitu ambapo walishirikiana kumuomba rushwa mfanyabiashara  wa mkaa mara baada ya kumkamata akiwa na maguni  50 ya mkaa.

Vilevile alisema kuwa uchunguzi wa Takukuru ulibaini kwamba fedha hizo zilipokelewa na Bw.Nassor Maulidy Mirambo Agoust 23 mwaka huu  kwa mikupuo miwili ambapo alipokea kwanza shilingi 250,000 kisha baadae akapokea kiasi cha Tsh.148,000 na baadae mfanyabiashara huyo aliweza kurudishiwa mkaa wake.

Sambamba na hayo mkuu wa takukuru mkoa alimalizia kwa kutoa lai kwa watumishi wa umma kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya rushwa vinginevyo watalipia kwa matendo yao wanayoyafanya
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad