Baba Ampa Mimba Mwanaye Kisa Kulala Karibu Naye

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wanafunzi watatu wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambao majina yao yamehifadhiwa wamelazimika kukatisha masomo yao baada ya kupatiwa ujauzito huku mmoja wapo akimtaja baba yake kuhusika na ujauzito wake.

Wote ni wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibuyuni iliyopo katika kijiji cha Mkuruwili, ambapo wawili kati yao ni wa darasa la saba na mmoja ambaye amemtaja baba yake wa kumlea kuhusika, ni mwanafunzi wa darasa la sita.

www.eatv.tv, imefika katika kijiji cha Mkuruwili na kuzungumza na wanafunzi hao ambao wanakiri kufanyiwa  unyama huo  huku mmoja wao akimtaja baba yake wa kufikia kuwa na tabia ya kumnyatia majira ya alfajiri pindi mama yake anapokwenda kuchota maji na kumlazimisha kushiriki tendo la ndoa huku akimtishia kumuua endapo atajaribu kumtaja.

Pia baadhi ya majirani wamesema kuwa sababu za mwanafunzi huyo wa darasa la sita kupewa ujauzito na baba yake wa kufikia ni kutokana na wazazi hao kulala kitanda kimoja na watoto wao.

Mwanafunzi mwingine aliyepewa ujauzito

Mwanafunzi mwingine amesimulia kuwa alibakwa na vijana wawili alipokuwa anakwenda shamba. Amesema walimvuta porini na kumfanyia kitendo hicho na alipopimwa shuleni na wenzake ndipo aligundulika kuwa na ujauzito.

Viongozi wa kijiji wanawazungumzijae wanafunzi hao

Kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo Bw. Warioba Joseph pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji wamekiri kutokea kwa tukio hilo huku wakieleza kuwa tayari hatua zimekwishaanza kuchukuliwa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad