10/04/2019

Basi la ILASI Express lagongana na Lori, Dereva afariki


Basi la ILASI Express lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya limegongana na Lori lililokuwa likitokea Iringa katika eneo la Kasanga, Morogoro na kusababisha kifo cha dereva wa lori papo hapo huku majeruhi 30 wakikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, kati ya hao wanaume 14 na wanawake 16.

Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali hiyo, Rita Lyamuya amethibitisha kupokea majeruhi hao ambapo amesema watatu kati yao wana hali mbaya na wawili wamepewa rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger