CHADEMA watoa Kauli kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawatasusia uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Novemba 24 mwaka huu na amewataka viongozi, wanachama na Watanzania kuhamasishana kujiandikisha.

Amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi ambapo ameeleza  uchaguzi huo ndio unawaleta viongozi wanaokwenda kutatua changamoto za wananchi hivyo kuacha serikali ifanye uamuzi ni kosa.

“Tunapaswa kuweka kando tofauti zetu, twendeni kwa wingi tukajiandikishe ili tushiriki kwenye uchaguzi huu muhimu,” amesema Mbowe

Ameendelea kwa kusema wananchi kusuasua kwenda kujiandikisha ni matokeo ya kile alichodai kuwa ni serikali  kuweka msisitizo katika kuwazuia watu wa upinzani kufanya mikutano ya kisiasa.

“Ni makosa makubwa na aibu kususia. Kwa muda wa siku tatu zilizoongozwa, viongozi wote wa kada zote, wahamasishane watoke kwa wingi kwenda kujiandikisha, hatuna sababu za kususia kwani tutakuwa tumesusia maisha yetu,” amesisitiza Mbowe

“Tunakwenda kushiriki uchaguzi huu na tutashinda, hatutakuwa woga na haya ni mapambano ya kisiasa, tutatumia nguvu za umma kuhakikisha tunashinda uchaguzi huu.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nimekuelewa mheshimiwa Mbowe lakini kwa mazingira ya kisiasa yalivyo ni ngumu vyama vya upinzani kushinda kwa sababu wasimamizi walishapewa maagizo ya kutowatangaza wapinzani hata wakishinda hiyo kauli imetukatisha tamaa wananchi, kususia siyo jambo zuri.

    ReplyDelete

Top Post Ad