Dalili 6 Zitakazokuonyesha Kuwa Mwenzi Wako Ana Mtu mwingine Katika Mahusiano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara, mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahusiano hayo huingia doa.

Watu kuwa na wapenzi wawili wawili huenda ikawa sijambo geni, lakini ni jambo geni pale mwezi wako akilifanya.

Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, lakini sidhani kama yatakuja kuzoeleka, maana kila mmoja hapa anahitaji upendo wa dhati na wakwake tuu, usio na kugawana na mtu mwingine.

Vitabu vya dini vinasisitiza upendo ulio mmoja katika mahusiano yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, 'tuliheshimu hili'.

Katika makala hii inayolenga kukuonyesha dalili za mwenzi wako kutoka nje ya mahusiano, kwa kiasi kikubwa itakusaidia wewe kuwa sehemu sahihi.

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mpenzi wako anamahusiano nje ya ndoa au urafiki wenu.

1. Mmekuwa wawazi kwa muda sasa, yani mwenzi wako amekuwa akishea na wewe mambo mbalimbali ya siku nzima, ghafla anaanza kuchelewa kurudi kutoka kazini, na akirudi hakuambii alikuwa wapi.

2. Umekuwa ukikaribishwa kumtembelea kazini kwake, lakini siku hizi anatengeneza sababu nyingi za kukuweka mbali na maeneo ya kazini kwake kabisaa.

3. Siku moja unapanda katika gari ya mkeo au mmeo alafu unataka kufungua kile kibox kilichopo pale mbele ambacho huwa kinatumika kuhifadhia vitu mbali mbali, mara unakuta kimefungwa kabisa na mwenzi wako anagoma kukifungua.

4. Ghafla mkeo/mme anaanza kujifungia bafuni anapokwenda kuoga, na hakuwa anafanya hivyo, je huenda akawa anatumia muda huo kuwasiliana na mtu mwingine kwa njia ya maandishi?

5. Mke/mme wako ana mikutano au mitoko na marafiki na kumbuka kukuhusu sehemu wanayokwenda inautata, mfano disco, bar usiku alafu hakuambii n.k.

6. Mpenzi wako anageuka kuwa msiri katika mambo yake, yani anakuficha nywila/passwod ya simu au laptop yake, tofauti na mwanzoni alikuwa anakuweka wazi.

Hayo na mengine mengi yanaweza kukufanya ukaona kuwa ni sehemu kubwa ya kuwa mumeo/mkeo anamahusiano na mtu mwingine nje ya mahusiano yenu.

Angalizo: Dalili zote hizo 6 huenda mpenzi wako akawanazo baadhi tu, kwa mfano kuchelewa kazini, usiri wa kazini n.k hii aimaanishi tu ni msaliti wa mapenzi, hapana wakati mwingine ziko sababu za msingi zinazo msababisha yeye kufanya hivyo na sio kuchepuka
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad