Kimenuka..Watumiaji wa Mtandao Wenye Video za Ngono za Kudhalilisha Watoto Wakamatwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kwa mujibu wa Wapelelezi, zaidi ya Watu 300 wamekamatwa kufuatia kugundulika na kufungwa kwa moja ya mtandao mkubwa wa udhalilishaji Watoto Duniani unaotengeneza video za ngono za Watoto

Mtandao huo uliofungwa mwaka jana na Uingereza baada ya uchunguzi dhidi ya wanaojihusisha na ngono kwa watoto kufanyika, ulikuwa na zaidi ya video 200,000 na zote kwa pamoja zilipakuliwa kwa zaidi ya mara Milioni

Jana, Maafisa wa Polisi wameeleza kuwa watu 337 wanaodaiwa kuwa walikuwa watumiaji wa mtandao huo wamekamatwa katika Nchi 38 tofauti huku mmiliki wa mtandao huo, raia wa Korea Kusini, Jong Woo Son (23) akiwa gerezani

Kwa Mujibu wa Maafisa hao, baadhi ya Nchi walipokamatwa Watuhumiwa hao ni Uingereza, Ireland, Marekani, Korea Kusini, Ujerumani, Uhispania, Saudi Arabia, the Umoja wa Nchi za Kiarabu, Jamhuri ya Czech na Canada

Mtandao huo uliokuwa unaitwa ‘Welcome to Video’ ulikuwa na Ukubwa wa tariban 8TB wenye maudhui ya kudhalilisha Watoto ambapo watu walikuwa wakinunua video hizo kwa kutumia safaru za kidijitali (Cryptocurrency)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad