Kingwangala "Tuwaache Watu WETU Wamsherehekee Rais, Huyu ni Mtu Wao Tusimtenge na Watu Wake"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Dr Kingwangala Ameandika Kupitia Ukurasa wake wa Instagram:

"Umoja wa watanzania umejengwa na kuimarishwa sana na ‘utani’ miongoni mwetu. Ndiyo maana tumeweza kuoleana na kufanya kazi kwa kiasi kikubwa bila kugombana ama kubaguana kati yetu. Mfano, kabila kubwa kama la kwetu ama la wasukuma tuna makabila watani zaidi ya 10 hapa nchini. Na ndiyo maana ilikuwa rahisi sana kuuza mgombea wetu mwaka 2015. Mgombea wetu alikuwa anataniana na kuongea/kusalimia kwa lugha za makabila karibu yote nchini ili kujisogeza karibu yao wamuone ‘mwenzetu’. Lakini pia Mhe. Rais wetu anapenda utani, wakati mwingine hutoa utani mbaya kabisa 😀, kama hujamzoea unaweza ukatafuta pa kuficha sura yako.

Watu wetu wa kila aina jana wamesherehekea birthday yake kwa upendo na Mshikamano wa kipekee. Nchi nzima imemuombea dua Rais wetu. Hali iliyoonesha kuwa kweli jana ni siku aliyozaliwa Rais Chuma/Jiwe tunayempenda. Birthday yake ilikuwa ya heshima, ya kiTaifa. Na miongoni mwetu wapo waliotania kuwa wanaenda ikulu kummwagia maji Rais, wengine walimwagia maji picha yake! Ilimradi tu kila mtu alisherehekea birthday ya Mheshimiwa kwa namna yake. Kuna watu wamekuwa wakiiga sauti ya Rais, wakiiga mavazi nk. Sidhani kama ni dhambi, zaidi kwa mwanamkakati kama mimi, nikifanya tathmini yangu, mara moja naona kuwa Rais anapendwa na watu wake.

Watu wanaona Rais ni mali yao. Wanajihusisha naye. Na hii ni dalili kuwa mwakani Rais atapita kwa upepo wa kisulisuli, pengine zaidi ya asilimia 90! My take: tuwaache watu wetu wamsherehekee Rais wao, huyu ni mtu wao, ni mali yao! Tusimtenge na watu wake. Imagine Rais angekuwa haleti utani hata kidogo, uso wa mbuzi mwanzo hadi mwisho, na sisi tukauona upande wake wa pili kwamba ni ‘binadamu’ mwenye utu, upendo na huruma, unadhani tungekuwa tunanyoosha mikono kumshauri kwa dhati kabisa kwenye vikao?! Kwanza tungezikimbia teuzi! 😀😀😀. Nani angebaki kumsaidia kazi hii ngumu aliyonayo? Utani wa Rais unalainisha vyuma kidogo. Tuwaache watanzania wamfurahie Rais wao jamani!" Kingwangala
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad