Makonda ajipa cheo kipya ili kukamilisha miradi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amejipa cheo kipya cha umeneja wa miradi wa mkoa huo, baada ya kukuta mradi wa ujenzi wa mto Ng'ombe wilayani Kinondoni kusimama, licha ya viongozi wa wilaya hiyo kumdanganya kuwa Mkandarasi yupo 'Site'.

Hayo yamejiri leo Oktoba 1, 2019 alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo  wilayani humo, ambapo akiwa katika mradi wa maboresho ya Mto Ng'ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ukiwa na urefu wa Km 7.5 ndipo alipobaini kuwa alifanyiwa mchezo mchafu na viongozi hao.

''Mimi ni  meneja mkuu wa miradi ya mkoa wa DSM, hiki ni cheo kipya cha mwezi wa kumi na nimekipata baada ya kuona mambo hayaendi tunavyotegemea, ukibaki na cheo cha ukuu wa mkoa utabaki kupokea taarifa ofisini, lakini ukiwa meneja miradi, utatembelea mradi wako kuanzia unajengwa hadi unakamilika'', amesema Makonda.

Kufuatia hali hiyo Makonda amewaonya watendaji wanaoendelea kumpa taarifa za uongo na kwamba yeye bado ataendelea kufanya ziara kwenye kila mradi ili kujionea kama taarifa anazoletewa kwenye karatasi zinaendana na kinachofanyika.

Akiwa kwenye mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la  Magomeni linalogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 8.9, Makonda amemtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha soko hilo linakabidhiwa Disemba mwaka huu.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndiyo inavyotaka Makonda.
    unaona mwenzako Mwanri / Ally Hapi
    Mh. Majaliwaa / Jafo / Waitara / Bashe
    na wenzao.
    Wote wako katika Medani kama Kama kipenzi chetu aivyo fungua Bati Vvinguguti juu ya Misumari kupigwa na kujiwekea Amani kuwa Hatoeza fika na Kafika na amejionea uzembe na wewe sasa Amka na usikae ofisini. Chacharika.

    ReplyDelete
  2. Ndiyo inavyotaka Makonda.
    unaona mwenzako Mwanri / Ally Hapi
    Mh. Majaliwaa / Kigwangalla / Jafo / Waitara / Bashe
    na wenzao.
    Wote wako katika Medani kama Kama kipenzi chetu aivyo fungua Bati Vvinguguti juu ya Misumari kupigwa na kujiwekea Amani kuwa Hatoeza fika na Kafika na amejionea uzembe na wewe sasa Amka na usikae ofisini. Chacharika.

    ReplyDelete
  3. Ndiyo inavyotaka Makonda.

  4. Ndiyo inavyotaka Makonda.Usimwangushe mteuzi wetu kwa kukuteua. Angaia mwenzako Aggrey Mwanri / Ally Hapi
    Mh. K.Majaliwaa / Kigwangalla / Jafo / Waitara / Bashe

Top Post Ad