Mganga wa kienyeji kizimbani kwa ubakaji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mganga wa kienyeji mkazi wa Ujiji Kigoma, Venas Edward (48), amefikishwa katika Mahakama ya wilaya mkoa wa Kigoma kwa madai ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka nane.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Katoki Mwakitalu, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na ameachiwa kwa dhamana.

Aliposoma maelezo ya awali, wakili wa Serikali alidai kuwa Aprili 23, mwaka huu majira ya asubuhi eneo la kasoko ujiji, mshtakiwa alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka nane na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Amedai siku ya tukio mtoto huyo alichukuliwa na mama yake mzazi na kwenda naye kwa mshtakiwa ambaye ni mganga wa kienyeji kwaajili ya kupata matibabu.

Baada ya kufika kwa mganga huyo mama wa mtoto aliambiwa aende kununua kiwembe dukani na kumuacha mtoto na mganga huyo, ambaye alitumia nafasi hiyo kumbaka mtoto.

Aidha upande wa mashtaka unatarajia kupeleka mashahidi watano pamoja kielelezo kimoja cha PF 3, na wameomba hakimu awapangie tarehe nyingine kwaajili ya kuanza kuwapeleka mashahidi.

Hakimu Mwakitalu alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9 kwa kusikiliza.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad