Rais Magufuli Afichua Siri ya Ukamataji Vigogo Waliopiga Bilioni 1.2 za Korosho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais John Magufuli amesema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inawashikilia viongozi wa vyama vya ushirika 92 mkoani Mtwara kwa tuhuma za kuwadhulumu wakulima wa korosho Sh. bilioni 1.2.

Amesema fedha hizo ni malipo ya korosho katika msimu wa mwaka 2016 hadi 2017, amewaahidi wakulima hao watalipwa fedha zao.

Aliyasema hayo jana, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akiwaapisha viongozi aliowateua mwishoni mwa wiki.

“Juzi nilikuwa Mtwara, Brigedia Jenerali Mbungo (Kaimu Mkuu Takukuru) anafahamu tulikuta malalamiko sana ya baadhi ya watu waliodhulumiwa malipo yao ya korosho kuanzia mwaka 2016 hadi 2017,” alisema na kuongeza:

“Na vilikuwa ni vyama vya ushirika 10, baada ya kumwagiza Brigedia Jenerali, akakuta ni vyama vya ushirika 32 ambavyo vilikuwa vinawadhulumu watu. Tulidhani walikuwa wamedhulumu Sh. milioni 80 tukakuta wamezdhulumiwa zaidi ya Sh. bilioni 1.2.”

Rais Magufuli alisema Takukuru imeweza kuwashika viongozi wa Amcos 92 na mpaka juzi walipokuwa wanampatia taarifa (Rais Magufuli) zilikuwa zimerudishwa Sh. milioni 255, na kwamba zilizobakia zinaendelea kurudishwa
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad