‘Mitazamo’ Mitatu ya JPM juu ya Shahada Aliyotunukiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya Rais Dkt. Joh Magufuli kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ameeleza jinsi alivyoipokea kwa furaha na kutoa mitazamo yake juu ya shahada hiyo.

Mtazamo wake wa kwanza ulianza kabla hajakubali wito wa kutunukiwa shahada hiyo ambapo ilimlazimu kujiuliza maswali mbalimbali na mwisho akapata jibu.

“Baada ya kuambiwa kwamba nitatunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa nilijiuliza maswali mengi, lakini nilikubali baada ya kukumbuka kuwa mara nyingi shahada hizi za heshima hazitolewi kwa maana ya kumpa mtu binafsi bali zinakuwa kwa niaba ya watu wengine,” amesema Magufuli.

Kaseja ataka lawama zielekezwe kwa wachezaji wote
Rais Dkt. Magufuli pia amesema anatambua kuwa shahada hiyo siyo yake binafsi bali ni ya watanzania wote, na huo ndiyo mtazamo wake wa pili juu ya shahada hiyo.

“Wakati napokea shahada hii ya heshima, kwa heshima, furaha, na unyeyekevu mkubwa, natambua kuwa si yangu binafsi bali ni ya Watanzania wote,” Ameeleza.


 Rais Magufuli amesema, “shahada hii kimsingi imetolewa kutokana na mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano, mafanikio hayo hayatokani na juhudi zangu binafsi bali kwa ushirikiano wa watanzania wote.”

Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli ni kiongozi wa tatu kutunukiwa shahada ya heshima kutoka chuo cha UDOM, baada ya Rais mstaafu, Jakaya kikwete na Waziri mkuu msataafu, Rashidi Kawawa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad