KIPA Manula Kibarua Kizito Mbele ya KASEJA...Wote Waitwa Stars

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


manula

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars',  Ettiene Ndayiragije amewaita wachezaji 32 kuunda kikosi kitakachoshiriki mashindano ya Chalenji yatakayofanyika Uganda.
Mashindano hayo ya Cecafa yataanza kutimua vumbi Disemba 7 mwaka huu huku kipa wa Simba, Aishi Manula akijumuishwa kikosini hivyo timu hiyo kuwa na makipa wanne wakiongozw ana Juma Kaseja wa KMC, Metacha Mnata (Yanga) na David Kisu (Gor Mahia ya Kenya).

Wachezaji wengine ni Salumu Kimenya, Mkandala Cleoface wote kutokea Tanzania Prison, Juma Abdul, Kelvin Yondan (Yanga), Gadiel Michael, Jonas Mkude, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Miraji Athumani kutoka Simba.

Wengine ni Mwaita Gereza, Zawadi Mauya, Yusuph Mhilu (Kagera Sugar), Fred Tangalu, Paul Nonga (Lipuli), Idd Seleman, Salum Abubakar, Shaban Chilunda(Azam), Baraka Majogoro na Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania).

Wengine Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union, Abdulmajid Mangalo (Biashara United),  Jafar Kibaya (Mtibwa Sugar) na Kikoti Lucas (Namungo).

Wachezaji watatu wanaocheza nje ya Tanzania walioitwa ni Nickson Kibabage wa Difaa El Jadid ya Morocco, Kelvin John kutokea Football House, Eliud Ambokile (TP Mazembe ya DR Congo) na Eliuter Mpepo (Buildcom Zambia).

Katika kikosi hiko Manula, amerejea baada ya kukosekana katika timu ya Taifa Stars, iliyocheza mechi ya kufuzu Chan na Afcon, wakati huo huo kuna sura mpya kama Abdul, Kikoti, Gereza, Ambokile, Kibabage, Mkandala, Mhilu, Nonga, Kibaya na Tangalu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad