Shamsa Ford na Nay wa Mitego Kunani Tena?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Moja kati ya video ambayo inazungumziwa kwa sasa ni ya muigizaji wa filamu Shamsa Ford na msanii wa muziki Nay wa Mitego, ikiwaonesha wakiwa dukani wakifurahi na kuongea kwa pamoja.

Video hiyo aliiweka Shamsa Ford, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ambapo aliandika.

"Kuachana si bifu jamani mnaachana kwa amani na upendo na kila mmoja amuombee kheri mwenzie, sisi vijana na tunategemeana kwenye kazi nyingi za kujenga Taifa letu, ahsante kwa kuja binamu yangu" ameandika Shamsa Ford.

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Shamsa Ford alipoulizwa kuhusu kama alikuwa anawasiliana na Nay wa Mitego, kipindi wameachana na hili ndilo jibu lake.

"Ndiyo, alinitania tu siku alivyosikia Ndoa yangu imeachika, akanipigia simu akaniambia 'Cousin' nasikia vitu vimeharibika huko" alijibu Shamsa Ford.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad