NAHISI Hili Jamaa Linachukua Msichana Wangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kuna huyu mwanadada ambae sasa ninafikisha miezi kadhaa tangu tuanze mahusiano, kiasi flani nimeridhika na tabia zake, tunaenda vizuri, yupo serikalini, amepanga upande wa nyumba ambayo wana share na jamaa mmoja hivi ambae pia ni work mate wake, mwenye hiyo nyumba ni bosi wao kazini, huko nyuma aliwahi kutangaza kazini kuwa ana nyumba ya kupangisha lakini ni ya ku share sababu ilikua designed for a single United family, ndipo akajitokeza msichana wangu na huyo jamaa kuihitaji hiyo nyumba, wamegawana vyumba ila sebule na jiko wana share.

Tatizo lenyewe ni hili;

Kitendo cha watu wa jinsia mbili tofauti kuishi mazingira kama hayo kimeni irritate mimi hivyo kusababisha magomvi ya kila mara kati yangu na msichana wangu, kwa sababu, wakati mwingine nikifika pale nawakuta wamekaa sebuleni wakitazama filamu huku lile jitu likiwa na boxer tu huku msichana wangu akiwa na night dress ingawa anakua kajifunga na kanga pia, halafu wakati wote msichana wangu ndie mpishi kwenye hiyo nyumba, hilo pumbavu limekaa kwenye sofa kusubiri chakula kama mme vile, huwa nikikuta hali hiyo naingiwa na hasira kali mno na tukiingia chumbani namuanzishia vagi msichana wangu.

Msichana huyu nilikua nimepanga kumuoa maana mimi pia umri wangu umesogea kidogo na wazee wamekua wakinisukuma sana kuhusu kuoa, ila mimi nilipanga nioe nikishajenga nyumba yangu jambo ambalo nilishalikamilisha mwaka Jana, nimekua nikimsihi huyu binti aondoke kwenye hiyo nyumba aje tuishi wote lakini hataki anasema hadi ndoa, jambo ambalo linanikasirisha maana mtu yupo tayari kuishi nyumba moja na hilo jitu lakini hataki kuishi na mimi Mchumba wake, hiyo ni haki kweli wadau?

Sasa inanilazimu mimi kwenda pale hata usiku wa manane kwenda kuchungulia tu hata madirishani bila wao kujua ili kuona kama usiku huwa wanajuana, wakati mwingine nalazimika kwenda kulala pale bila kupenda katika mazingira ya hofu,
lakini yote hayo ni tisa, kumi, lile jitu huwa halinipendi, nikifika pale linaondoka, likiniona mimi nimefika pale, hata kama lilikua limevaa nguo litaenda kuvua linakua linapitapita hapo na boxer tu huku nyeti zake zikionekana wazi ku swing kwenye boxer, haliongei na mimi wala story tu za udugu kama watanzania tulivyozoeana,
i mara zote nikianzisha mada hii msichana wangu hunitoa wasi wasi kuwa hamna chochote kinachoendelea kati yao, na kwamba ni wasi wasi wangu tu, na kwamba anamheshimu tu kama kaka yake na ndio maana humpikia na kumfulia wakati mwingine, mimi siamini.

Ngoja niishie hapa, kwa kweli nina hasira sana, hivi kwa jinsi nilivyowaeleza mnadhani kuna chochote kinaendelea kati ya msichana wangu na hili jitu behind my back?

Tusaidiane wadau
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad