Ndoa ni DIRECT VISA To Hell Kama Ukiichukulia Poa, Ni Heri Usioe ama Kuolewa Kama Humaanishi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kila mtu anataka Kuolewa lakini shida ni Vigezo vya Waoaji vikoje??Kila siku vigezo vinabadilika..Sasa hivi unaangaliwa sana uwezo wako wa mfukoni kabla hujaambiwa NDIO...Hela imekuwa ndo GREEN LIGHT,ukiwa hohehahe basi utazungushwa wee na utaambiwa kila siku,"IAM NOT READY FOR MARRIAGE"
Kuna watu wametoswa kisa Wallet hazisomi na ukashangaa wameolewa na watu kisa WANA HELA..
Hela ingekuwa kila kitu AMBER ROSE na WIZ KHALIFA wasingeachana..Wana kila kitu wale...
Hela ingekuwa jawabu NICK CANNON na MARIAH CAREY wasingeachana...
Hela ingekuwa kila kitu JASON DERULLO na JORDIN SPARKS wangekuwa happily married lakini Wapi...
Raha ya ndoa itoke Moyoni...Mpendane kwa jinsi mlivyo...Mpendane kwa hali yoyote mliyonayo na muelewane..
Kuna watu kula kwao ni kwa mbinde lakini ndoa yao ina amani na furaha mwaka wa 20 huu...Kuna watu wana kila kitu,Magari,Mashamba,Viwanja,Akaunti zilizonona lakini hata miaka 3 wameshindwa kufikisha...Wamekuwa WATALAKA VIJANA...
Ndoa ni DIRECT VISA to Hell kama ukiichukulia poa,ni heri Usioe ama kuolewa kama humaanishi...Maana ukiachana na mwenza wako ndani ya miaka 3 hiyo miaka mingine yoooteee UNAZINI TU...Mbingu utaisikia kwenye kipindi cha JAHAZI tu...
Jifunze kwa Wajane na Watalaka...Jua unachotamani na UJIPANGE!

By Seth
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli kabisa, ndoa sio utajiri, ndoa ni upendo wa kweli kutoka moyoni. Ukimpenda mtu kutoka moyoni hutaangalia ana kitu gani, ukiolewa kwa sababu ya utajiri, utajiri ukiisha na ndoa nayo inaisha. "NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE". KILA MTU ASEME AMEN

    ReplyDelete
  2. Utakuta hili gauni maBiharusi woote wanaazimana hapo kijijini.

    ReplyDelete
  3. Kwasababu pesa unakuwa ushapata kwa ticket ya ndoa na tajiri ila huitaji wako wa mwenza wa maisha umpendae ambaye kemikali zenu hujichanganya vizuri au sumaku zenu huvutana kaskazini kwa kusini unakuwa bado haujapata majibu. Hivyo unakuwa na mtu ndani ya nyumba na pesa na mali nyingi wakati moyoni kuna shimo linalohitaji mwenza ambaye hujampata ingawa kwa watu na kwenye makaratasi wewe ni mke wa mtu. Hiyo ndio inafanya bado usiwe na furaha ya huo uhusiano hata kama mwenzako hajakuudhi. Na ikitokea tu kskosea kidogo, unakuwa umeshapata warrant ya kukutoa nje ya ndoa hiyo, sababu hakuna binadamu asiyekosa. Pia huyo mwenza naye anajikuta naye hajapata matarajio yake, kwani alifikiri kapata kumbe mambo ni tofauti. Anajiuliza nimekosea wapi na hapati jibu na haoni kemikali au sumaku ya kuvutana. Ameshasaini na kuapa kaoa, lakini kiuhalisia huitaji wake wa mke upo vilevile kama awali kabla hajaapa. Na sasa mbaya zaidi hawezi kutafuta mchumba tena, yupo kifungoni na mtu ambaye hamuoni kama yeye ni mume. Heri kumhusisha Mungu na kuwa na subira kabla ya kuingia kwenye ndoa na kupendelea kuombea ndoa kila leo

    ReplyDelete

Top Post Ad