AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Wafanyakazi wanne wa kampuni ya uwindaji ya Green Miles iliyoondolewa katika kitalu cha Lake Natron(east) wilayani Longido wanashikiliwa na polisi kwa madai ya kukaidi agizo la Serikali kuondoka wa hiari katika kitalu hicho.
Wafanyakazi hao wamekamatwa na polisi leo Jumatano Januari 22, 2020 waliokuwa wameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Longodo mkoani Arusha.
Wanatuhumiwa kuendelea na kazi katika kitalu hicho licha ya kutakiwa kuondoka Januari 20, 2020.
Katibu tawala Wilaya ya Longido, Toba Nguvila amesema baada ya wafanyakazi hao kukamatwa, eneo hilo litakuwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) kwa kushirikiana na polisi.
Ofisa wanyamapori wa kikosi cha kuzuia ujangili Mkoa wa Arusha, Emmanuel Pius amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni kaimu meneja wa kambi ya Tandala, Lazaro Lembrise, Moses Sikange, Mohamed Bembe na Hassan Mahonza.
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK