Maambukizi ya virusi vya Corona yapindukia 70,000

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Idadi ya walioambukizwa virusi vya Corona kote nchini China imepindukia watu sabini elfu. Kulingana na maafisa wa afya, idadi ya vifo kutokana na virusi hivyo imeongezeka na kufikia watu 1,770.

Kulingana na tume ya afya nchini China kulikuwa na zaidi ya maambukizi elfu mbili na vifo vya watu 105 katika kipindi cha masaa ishirini na nne. Idadi hiyo ya waliofariki jana Jumapili inaonekana kwenda chini kidogo ikilinganishwa na Jumamosi ambapo watu 142 walifariki, huku idadi ya walioambukizwa ikidaiwa kuongezeka kidogo.

Hapo jana mkoa wa Hubei ambao ndio kitovu cha virusi hivyo ulianzisha hatua nyengine kali zaidi zinazolenga kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

Hatua hizi mpya zinajumuisha kuendelea kuwadhibiti watu wasitoke nje kwa masaa ishirini na nne na pia kuweka marufuku ya magari yote barabarani isipokuwa yale yanayotoa huduma za dharura.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad